Burudani

Sholo Mwamba, Diamond wafuta wizi, udangaji na uteja Tandale

DAR ES SALAAM: MSANII wa singeli Sholo Mwamba amesema mafanikio wanayopata yeye na Diamond Platinumz katika muziki yamebadilisha hadhi ya Tandale kwa vijana wa sasa togauti na ilivyokuwa zamani.

Sholo Mwamba amesema Tandale kulizoeleka kwa sifa mbaya ya wizi, udangaji, uteja na mambo mengi ya hovyo lakini kupitia mafanikio yao kimuziki imejenga wivu mzuri kwa vijana wa sasa ambapo wengi wao wameachana kujihusisha na mambo mabaya badala yake wanafanya muziki na shughuli nyingine tofauti na uharifu.

“Tandale ilikuwa mbaya ukizaliwa kule ilikuwa ukikosa kuwa teja (mtumiaji dawa za kulevya) unakuwa mwizi, mkabaji na kwa wanawake wanakuwa wadangaji, ubaya wote ulikuwepo Tandale lakini kwa sasa Mungu ni mwema vijana wengi wanatuiga mimi na Diamond wanafuata tunachofanya wameachana na matukio ya hovyo,” Sholo Mwamba.

Sholo Mwamba aliongeza kwamba ndoto ya kwanza ya kuwabadilisha vijana wa Tandale inatimia kwa kuwa amekuwa mfano mzuri wa kuigwa na vijana wengi kupitia muziki wake.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button