Burudani

Domokaya: Wasanii tusibaguane

MSANII mkongwe wa muziki wa Bongo Fleva, Domo Kaya amewaomba wasanii wenzake kuacha tabia ya kubaguana kutokana na nyakati walizopo.

Domo Kaya alisema kumekuwa na tabia za wasanii wa sasa kukataa kushirikiana na wakongwe katika nyimbo zao wakihofia kutofanya vizuri kimauzo.

Domo Kaya aliyewahi kuwika na msanii mwenzake Man Dojo wakitamba na wimbo wa ‘Nikupe nini’ mwaka 2002 na ‘Dingi’ mwaka 2004, alisema wasanii wazamani wamekuwa wakipitia wakati mgumu wanapotaka kurudi upya katika muziki kutokana na wasanibkutengana kimatabaka ya nyakati zilizopo na zilizopita.

“Kuna mambo yanaendelea hayajengi kwa wasanii msanii mkonhwe kama mimi unaweza kutaka kufanya kolabo na wasanii wenye mafanikio kwa sasa wanakataa wanasingizia ratiba zao zinawabana wanatukosea wakongwe,” alisema Domo Kaya

Related Articles

Back to top button