Kwingineko

Alvaro Carreras, Mbappe kuwakosa Manchester City

MADRID, Hispania: Klabu ya Real Madrid imethibitisha kuwa beki wake Álvaro Carreras na Kylian Mbappé wataukosa mchezo muhimu wa Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Manchester City utakaochezwa kesho Jumatano.

Kwa mujibu wa taarifa ya klabu hiyo, Carreras amepata majeraha ya misuli mguu wake wa kulia, hali itakayomlazimu kukaa nje ya uwanja kwa muda ambao bado haujabainishwa.

Huku mshambuliaji nyota Kylian Mbappé akidaiwa kutokuwepo kwa sababu hakushiriki mazoezi ya timu siku ya Jumatatu huku akiendelea kupona maumivu ya goti yaliyomsumbua tangu Desemba mwaka jana.

Mbappe, ambaye ndiye kinara wa mabao wa Madrid msimu huu, anatarajiwa kuukosa mchezo huo utakaopigwa katika dimba la Santiago Bernabéu Stadium dhidi ya kikosi kinachoongozwa na kocha Pep Guardiola.

Mbali na Mbappe, Madrid pia inakabiliwa na majeruhi kadhaa akiwemo Jude Bellingham, Éder Militão, Rodrygo Goes, Dani Ceballos na David Alaba ambao bado wanaendelea na matibabu.

Ripoti za vyombo vya habari vya Hispania zinaeleza kuwa Mbappe anatarajiwa kurejea uwanjani katika mchezo wa marudiano utakaochezwa wiki ijayo.

Related Articles

Back to top button