Thea aigeukia Injili
DAR ES SALAAM: Msanii wa filamu nchini, Salome Ndumbagwe Misayo, ‘Thea’ ameamu kuigeukia Injili na kuachana na maisha yake ya awali na kuishi maisha ya kumpendeza Mungu.
Akizungumza leo jijini Dar es Salaam amesema ametambua kuwa hata uwe nani unatakiwa kuishi maisha ya kumpendeza Mungu kwa kujifunza neno lake litakalofanya maisha yako kuwa barua inayosomeka kwa kila mtu.
Thea amesema kuwa ataungana na waumini wa kanisani kwao katika Kongamano la siku tatu kuanzia Agosti 26 ha 28 katika kanisa la Kiluther Afrika Mashariki. Kongamano hilo litaambatana na ufunguzi wa kanisa hilo.
“Lengo ni kutoa neno litakalotusaidia kuishi vizuri na wenzetu katika kila jambo na mwishoni tuweze kuwa na mwisho mwema kwenye maisha yetu ya kila siku.”amesema Thea