Kwingineko

Mbappe amjibu Neymar madai ya wivu kwa Messi

KYLIAN Mbappe ameonesha kutopendezwa na madai ya Neymar kuwa alionesha wivu kwa Lionel Messi wakati walipokuwa wakicheza pamoja Paris Saint-Germain (PSG).Wiki iliyopita akifanya mahojiano na Romario, Neymar alidai kuwa uhusiano wake na Mbappe ulianza kuharibika Messi alipojiunga na PSG

Akijibu madai hayo kupitia TNT Sports Brazil, Mbappe alisema: “Sina cha kusema. Namheshimu Neymar, ni mchezaji wa kipekee katika historia ya soka. Ninakumbuka nyakati nzuri tulizoshirikiana Paris, lakini sasa nipo Real Madrid na nataka kujikita hapa. Namtakia kila la heri Neymar, familia yake, na marafiki zake wote.”

Mbappe kwa sasa anang’ara akiwa na Real Madrid, huku Neymar akiichezea Al-Hilal nchini Saudi Arabia na Messi yupo Inter Miami.

Mbappe atarejea uwanjani leo Januari 22, 2025 kuiongoza Real Madrid dhidi ya RB Salzburg katika Ligi ya Mabingwa, wakisaka ushindi muhimu wa kuimarisha nafasi yao kwenye hatua ya mtoano.

Related Articles

Back to top button