Nyumbani

Azam FC yaifuata Wydad kusaka robo fainali

DAR ES SALAAM: KIKOSI cha wachezaji 25 wa Azam FC kimeondoka mapema leo kuelekea Morocco kwa ajili ya mchezo wa mwisho wa hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Wydad Athletic Club, utakaopigwa Jumapili.

Mchezo huo unasubiriwa kwa hamu kubwa kwani ndio utakaoamua hatma ya Azam FC katika michuano hiyo.

Azam FC inashika nafasi ya tatu kwenye kundi ikiwa na pointi tisa, sawa na Maniema Union ya DR Congo, huku vinara Wydad wakiongoza kwa pointi 12.

Licha ya kupewa nafasi ndogo ya kufuzu, Kocha Mkuu Florent Ibenge amesema kikosi chake hakijakata tamaa na kiko tayari kupambana ili kupata matokeo mazuri.

Matokeo ya michezo yote ya mwisho ya makundi ndiyo yatakayoamua timu zitakazofuzu hatua ya robo fainali, huku Nairobi United ikiwa tayari imeshaaga mashindano hayo.

Related Articles

Back to top button