Ligi KuuNyumbani

Simba harakati nafasi ya pili

KLABU ya Simba leo inashuka dimbani ugenini jijini Dodoma kuikabili Dodoma Jiji katika harakati za kuwania nafasi ya pili ya Ligi Kuu Tanzania Bara.

Simba ipo nafasi ya tatu katika msimamo wa ligi ikiwa na pointi 57 baaada ya michezo 26 nyuma ya Azam yenye pointi 60 baada ya michezo 27.

Klabu hiyo ya Msimbazi ina nafasi ya kushika nafasi ya pili iwapo itaifunga Dodoma Jiji zaidi ya mabao 3 kwenye uwanja wa Jamhuri.

Tayari Yanga imetwaa ubingwa kwa msimu wa 2023/2024 baada ya kufikisha pointi 71 ambazo haziwezi kufikiwa na timu yoyote wakati ligi itakapofikia tamati Mei 28.

Related Articles

Back to top button