KOCHA msadizi wa JKT Tanzania George Mketo amesema klabu yake imejiandaa vizuri kuufungua uwanja wao wa Meja Jenerali Isamuhyo kwa ushindi dhidi ya Simba.
Alikuwa akizungumza leo wakati wa mkutano wa waandishi wa habari kuelekea mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara kati ya timu hizo Februari 15.
“Kitu cha pekee na cha faraja zaidi ni kupata nafasi kucheza kwenye uwanja wetu wa nyumbani,” amesema Mketo
JKT Tanzania imehamishia michezo yake Meja Jenerali Isamuhyo uliopo Mbweni, Dar es Salaam kutoka Azam Complex.