Nyumbani
Singida BF kuivaa AS Vita
SINGIDA Fountain Gate itakipiga dhidi ya klabu ya AS Vita katika mchezo wa kirafiki Agosti 2.
Siku hiyo itatumika kutambulisha wachezaji na benchi la ufundi la timu hiyo iliyokuwa ikiitwa Singida Big Stars.
“Mchezo wenye hadhi ya kimataifa Rasmi. Tutacheza na AS Vita Club ya DR Congo kwenye kilele cha siku kubwa ya #SingidaBigDay tarehe 02/08/2023 katika Dimba la Liti stadium hapa mjini Singida,” imesema taarifa ya timu hiyo.
Tayari Yanga imefanya Wiki ya Mwananchi Julai 22 yenye lengo kama hilo huku Simba Day ikipangwa kufanyika Agosti 6.