Africa

Masanza: Singida hakuna kulala Zanzibar

ZANZIBAR: SINGIDA Black Stars imesema haina muda wa kupumzika tayari imewasili Zanzibar tangu jana ikitokea Jamhuri ya Congo, ikianza mara moja mazoezi ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya CR Belouizdad ya Algeria.

Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Jumapili kwenye Uwanja wa New Amaan Zanzibar.

Akizungumzia maandalizi ya mchezo huo, Ofisa Habari wa Singida Hussein Masanza alisema mara baada ya kuwasili visiwani humo, timu ilianza mazoezi na imeendelea na programu ya maandalizi leo, akisisitiza kuwa lengo ni kurejea kwenye mstari baada ya matokeo yasiyoridhisha katika mchezo uliopita wa hatua ya makundi.

Singida Black Stars ilipoteza mchezo wake wa mwisho wa hatua ya makundi kwa mabao 2-1 dhidi ya AS Otoho ya Jamhuri ya Congo, matokeo ambayo Masanza amesema yamewaumiza lakini yameongeza ari ya kupambana katika mchezo unaofuata.

“Mchezo unaofuata ni muhimu sana kwetu. Ni mechi ya kisasi kwa sababu walitufunga mabao 2-0 kule kwao, hivyo tunaingia tukiwa na dhamira ya kulipa kisasi,” alisema Masanza.

Alisema CR Belouizdad si timu ya kuogopa kupita kiasi, akisisitiza kuwa Singida Black Stars ina uwezo wa kupata matokeo mazuri endapo itajiandaa vizuri.

“Tunaamini tunawamudu. Wameshawahi kufungwa na Simba na Yanga, hivyo hata sisi tukijipanga vizuri, tukacheza kwa nidhamu na kujituma, tunaweza kuwafunga,” aliongeza.
Mwisho

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button