Africa
Al Ahly yaimaliza Medeama
KLABU ya Al Ahly leo imefifisha matumaini ya Medeama kutinga hatua ya 8 bora Klabu Bingwa Afrika baada ya kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya timu hiyo ya Ghana.
Bao hilo la Al Ahly kwenye mchezo huo wa kundi D uliofanyika uwanja wa michezo wa Baba Yara, Kumasi Ghana limefungwa na Hussein El Shahat katika dakika ya 48.
Al Ahly imefikia pointi 9 baada ya michezo 5 wakati Medeama imebaki na pointi 4.
Katika mchezo mwingine wa kundi hilo Februari 24 Yanga yenye pointi 5 itashuka dimba la Benjamin Mkapa kuikabili CR Belouizdad ya Algeria pia yenye pointi 5.(Picha:Al Ahly SC)