EPLKwingineko

Lopetegui kocha mpya Wolves

KLABU ya Wolverhampton Wanderers imemteua Mhispania Julen Lopetegui kuwa Kocha wake mpya baada ya awali kukataa.

Lopetegui mwenye umri wa miaka 56 atachukua mikoba Novemba 14 wakati Ligi Kuu ya Uingereza(EPL) itakaposimama kupisha fainali za Kombe la Dunia zitakazoanza Novemba 20, Qatar.

“Julen ni kocha wa kiwango cha juu, mwenye uzoefu wa kipaji cha kusoma mchezo,” amesema Mwenyekiti wa Wolves Jeff Shi.

Mechi ya kwanza ya Lopetegui EPL itakuwa Desemba 26 ugenini dhidi ya Everton.

Kocha huyo wa zamani wa Real Madrid alitimuliwa kazi Sevilla baada ya kufundisha kwa miaka mitatu kufuatia kichapo katika mchezo dhidi ya Borussia Dortmund Oktoba katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Related Articles

Back to top button