Ligi Ya Wanawake

Yanga Princess kulikoni!

DAR ES SALAAM: YANGA Princess ni miongoni mwa timu sita hazijashinda mchezo wowote Ligi Kuu soka ya Wanawake katika mizunguko mitatu waliyocheza.

Matokeo wanayopata wanaonekana kujitenga taratibu na wapinzani wao wakubwa Simba na JKT Queens ambao wanaoongoza nafasi ya kwanza na pili huku Yanga ikiwa nafasi ya sita, wakiachana kwa tofauti ya pointi nne mpaka sita.

Katika michezo mitatu waliyocheza hajawapoteza mchezo wala hawajashinda bali yote wametoka sare.

Timu hiyo inashika nafasi ya sita kwa pointi tatu pointi sawa na Gets Program nafasi ya tano na Bunda Queens wan ne, Mashujaa wa tatu pointi tano, JKT Queens pointi saba na Simba Queens kinara kwa pointi tisa.

Ukiacha Yanga Princess ambao hawajashinda mchezo wowote, wengine ni Bunda Queens wenye sare tatu, sawa na Gets program huku Alliance Girls katika michezo miwili ikipata sare moja na kupoteza mmoja, Mlandizi Queens wameshinda mmoja, wamepoteza miwili na Fountain Princess wakipoteza miwili katika michezo miwili.

Yanga Princess inakwenda kukutana mchezo ujao dhidi ya Simba Queens ambao mara ya mwisho walikutana kwenye ngao ya jamii na Yanga kushinda kwa penalti 4-3 kufuatia sare ya bao 1-1 ndani ya dakika 90.

Mchezo huo ujao utachezwa Novemba 12, mwaka huu kwenye Uwanja wa KMC.

Related Articles

Back to top button