Yamal afanyiwa Sherehe ya kuimaliza England leo

UJERUMANI: MCHEZAJI nyota mwenye umri mdogo anayeitumikia timu ya taifa la Hispania Lamine Yamal jana amefanyiwa sherehe ya siku yake ya kuzaliwa akitimiza miaka 17 huku wachezaji wenzake wakimpa maneno ya matumaini kuelekea fainali ya Euro 2024 dhidi ya England.
Wachezaji hao pamoja na wanahabari wa kihispania wamesema sherehe hiyo itaendelea kubaki katika mioyo yao endapo watafanikiwa kuifunga Uingereza na kubeba kombe la Euro 2024 leo usiku.
Winga huyo amekuwa akiweka rekodi mbalimbali tangu acheze kwa mara ya kwanza katika timu ya taifa ya Hispania mnamo Septemba 2023 na kuwa nyota mdogo aliyeibuka kwa mafanikio katika mashindano ya Euro 2024.
Sherehe hiyo kubwa nchini Hispania baada ya kuripotiwa katika vyombo mbalimbali vya habari kwa wachezaji waliopo Ujerumani wameisherehekea kwa kukata keki kubwa iliyojazwa mishumaa huku wakiimba wimbo wa kumpongeza Lamine kutimiza miaka hiyo 17.
Yamal alitoa hotuba fupi kwa wachezaji wenzake, akisema: ‘Nina furaha sana kutumia siku yangu ya kuzaliwa hapa Ujerumani na kwenda fainali na ninyi nyote, nataka kushinda kombe hili mbele ya England.”
Mara ya mwisho Hispania kubeba kombe hilo ilikuwa mwaka 2012, wakati kinda Yamal alipokuwa na umri wa miaka mitano tu.