Tetesi
XAVI: Messi ? simu moja tu

SAA 1 na dakika 55 na umbali wa Km 831 atautumia ‘La Pulga’ kutoka Paris hadi Catalunya Camp Nou baada ya mkufunzi wa ‘Blaugrana’ Xavi Hernandez kuthibitisha kuwasiliana na Muagentina huyo akiwa kipaumbele cha Barca.
Taarifa iliyotolewa na mwandishi wa habari na michezo, Fabrizio Romano imesema kuwa Xavi amewasiliana na Lionel Messi ‘La Pulga’ amemueleza kwamba maamuzi ya mwisho yamebaki kwa kwake.
“Vipaumbele viko wazi sana. Ningependa sana Messi arejee, nimezungumza naye nimeshasema kwamba inategemea yeye”. Amesema Xavi.
Wakati Xavi akisema hayo, zipo taarifa kwamba Messi amefanya mazungumzo na Al-Ittihad ya Saudia kwa ajili ya kuitumikia timu hiyo.