Tetesi
Jorginho, Partey milango ipo wazi

LONDON: KOCHA wa Arsenal, Mikel Arteta, amesema Jorginho na Thomas Partey wanaweza kuondoka kabla ya dirisha la usajili la Januari kufungwa. Wachezaji hao wawili wana miezi chini ya sita kwenye mikataba yao na wanaruhusiwa kujadili uhamisho wa bure majira ya kiangazi.
Arteta amesema kuna mawasiliano ya karibu kati ya klabu na wachezaji hao kuhusu mipango yao na maamuzi yanaweza kufanyika hivi karibuni.
Jorginho, mwenye umri wa miaka 31, na Partey, mwenye miaka 33, ni miongoni mwa wachezaji wanaolipwa mishahara mikubwa zaidi Arsenal. Hivyo, katika kuhakikisha klabu inapunguza matumizi makubwa ya fedha kulipa mishahara klabu hiyo inasemekana kuwafuatilia viungo chipukizi kama Jobe Bellingham wa Sunderland na Lucien Agoume wa Sevilla kama mbadala wa muda mrefu.