Tetesi

Casemiro, Varane, Sancho huru kuondoka

Manchester United iko tayari kusikiliza ofa za kuwasajili kiungo mbrazil Carlos Henrique Casimiro, maarufu Casemiro,31, beki mfaransa Raphael Varane, 30, na winga wa England, Jadon Sancho, 23, wakati kocha Erik ten Hag anajaribu kupunguza kikosi chake. (Independent)

Beki wa kati wa Everton, Jarrad Branthwaite, 21, na beki wa Crystal Palace, Marc Guehi, wako kwenye orodha ya kocha Ange Postecoglou ya wachezaji wanaohitajika zaidi wakati kocha huyo wa Tottenham akifanyia mabadiliko kikosi cha timu hiyo.(Sky Sports)

Fulham imeweka wazi kuwa kiungo mbrazil wa Fluminense, Andre, 22, ni kipaumbele chake namba moja cha usajili iwapo kiungo mreno Joao Palhinha, 28, ataondoka Craven Cottage Januari, 2024. (Telegraph – subscription required)

Manchester United na Newcastle United sasa zinaongoza mbio kumsajili fowadi wa Guinea,  Serhou Guirassy, 27, kutoka Stuttgart.(Football Insider)

Klabu ya Ligi Kuu Marekani, MSL, Colorado Rapids iko katika mzungumzo kuhusu kumsajili golikipa wa Marekani Zack Steffen, 28, anayekipiga Manchester United.(Athletic – subscription required)

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button