Filamu

Watengeneza filamu watakiwa kusimulia filamu za Afrika

ZANZIBAR: WATENGENEZAJI filamu wa Kiafrika wametahadharishwa kwamba kama hawatotengeneza filamu zenye hadithi za kweli kuihusi Afrika wasilahumu watengenezaji wa filamu kutoka mataifa mengine watakapo tengeneza filamu hizo kwa namna wanavyotaka wao.

Kauli hiyo imetolewa na washiriki wa mjadala wa umuhimu unaokua wa Hadithi za Kiafrika ulioendeshwa na Tamasha la Filamu la Kimataifa la Zanzibar (ZIFF) leo asubuhi katika Hoteli ya Serena, Unguja Jijini Dar es salaam.

Watengenezaji filamu wengi wameelezea changamoto kubwa ya kukosekana kwa fedha za kutosha zinazowawezesha kutengeneza filamu kutokuwa na mtazamo wao halisi kwa sababu ya ukosefu wa bajeti ya kufanyia filamu hizo na wanapoomba misaada wanatakiwa kufuata masharti ya wafadhili jambo ambalo linaharibu uhalisia wa hadithi za Afrika na kupotosha maana halisi ya Afrika.

Katika kuthibitisha hayo Mgolomba alitolea mfano wa filamu iliyotengenezwa nchini Afrika Kusini iliyokuwa inajadili masuala ya jando baada ya kukosa bajeti walipewa ufadhili wa masharti kwamba waongeze mashoga katika hadithi hiyo hali iliyokemewa vikali na wadau mbalimbali kutoka afrika sababu wameharibu uhalisia wa simulizi nzima ya afrika ambayo inapoinga vitendo hivyo.

“Huu ni mfano halisi wa upotoshaji filamu, Afrika Kusini ililazimishwa kuingiza maudhui ya ushoga katika simulizi iliyokuwa ikihusu utamaduni wa jando. Watayarishi wa filamu walikumbana na shinikizo la kubadilisha hadithi yao halisi ili kukidhi matakwa ya wafadhili, jambo lililosababisha maudhui yaliyokwenda kinyume na mila na desturi za jamii husika,” Amesema Mgolomba.

Mjadala umesisitiza umuhimu wa kukuza tasnia ya filamu barani Afrika ili iweze kujitegemea kifedha na kimtazamo. Paneli imetoa wito kwa serikali, taasisi za kitamaduni, na wawekezaji binafsi kutoa kipaumbele kwa sekta hii. Ni kupitia uwekezaji thabiti na uelewa wa kina wa umuhimu wa kusimulia hadithi zetu wenyewe ndipo Afrika inaweza kufaidika kikamilifu na utajiri wa simulizi zake.

Cece naye alisema kwamba pamoja na nia ya kufanyua masimulizi na kuonghezeka kwa hadithi zilizosimuliwa na waafrika wenyewe katika tamasha kubwa kama la cannes bado tatizo la raslimali fedha ni kubwa na kuna wakati mbunifu anashangaa kama ile hadithi ni yake au ya yule aliyetoa fedha.

Dk Mona katika mazungumzo hayo alisema kwamba usimuliaji wa hadithi ni ule ule ila watrengeneza filamu wa Kiafrika ni lazima kutafuta namna ya kubaki kama wasimuliaji bila kuingilia na wageni kwa kuwa na mazungumzo yenye tija yanayojali maslahi ya Waafrika na masimulizi yao.

Mjadala umesisitiza umuhimu wa kukuza tasnia ya filamu barani Afrika ili iweze kujitegemea kifedha na kimtazamo. Paneli imetoa wito kwa serikali, taasisi za kitamaduni, na wawekezaji binafsi kutoa kipaumbele kwa sekta hii. Ni kupitia uwekezaji thabiti na uelewa wa kina wa umuhimu wa kusimulia hadithi zetu wenyewe ndipo Afrika inaweza kufaidika kikamilifu na utajiri wa simulizi zake.

“Ikiwa hatutasimulia hadithi zetu wenyewe, pengo hili litajazwa na wengine, ambao huenda hawana uelewa sahihi wa tamaduni zetu, historia zetu, na matarajio yetu. Matokeo yake yanaweza kuwa filamu zinazopotosha ukweli, kuimarisha dhana potofu, au hata kuharibu taswira halisi ya Afrika.” alisema Dk Mona

Mjadala huo umewajumuisha wataalamu wa masuala ya filamu akiwemo Mwenyekiti, Bodi ya Filamu Tanzania Dkt. Mona N. Mwakalima, Mtayarishaji/Mkurugenzi, MASRAX, Somalia, Abdulkadir S. Mohamed, Mkurugenzi, Tamasha la Filamu la Eastern Cape, Nceba Mgolomba na Mtengeneza Filamu na Msimamizi wa Ubunifu, Kijiweni Productions, Cece Mlay na umeendeshwa na Msimamizi wa Tamasha la Filamu la Uganda, UCC, Leonard Amanya.

Related Articles

Back to top button