‘Wasanii mshindwe wenyewe’!

DAR ES SALAAM: WASANII mbalimbali wametakiwa kujitokeza kupima ugonjwa wa moyo na kupatiwa matibabu bure kwa muda wa miezi miwili Desemba 21 hadi Januari Kawe Mkapa Plaza jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Dk Peter Kisenge amesema kuwa amesema kuwa lengo ni kuwasaidia wasanii wasiwe na magonjwa yasio ambukiza.
“Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dk Samia Suluhu ametaka wasanii wa filamu, bongo fleva na sanaa mbalimbali kupatiwa vipimo vya magonjwa ya moyo ili kuepuka magonjwa yasio ambukiza.
“Zoezi la upimaji litaanza rasmi Disemba 2024 hadi Januari 2025 kila siku ya jumamosi na Jumapili kuanzia asubuhi hadi jioni wasanii watakuwa wakichekiwa afya zao katika ugonjwa wa moyo.
“Baada ya wasanii wengi kupatiwa na matatizo ya moyo wazo lilikuja nikamshirikisha Steve akasema jambo jema na Mama akaliunga mkono leo tunaangazia rasmi wa wasanii kuja kupimwa.
Kwa upande wake Steve Mengere maarufu kama ‘Steve Samia’ amesema kuwa watu wasiwe na kipaumbele kuchangia misiba tu bali hata matibabu, Mama analea watoto wengi na hili ametupa kipaumbele wasanii.
“Nafasi imetolewa ni kitendo cha Msanii kutoka kwake na kwenda kupima afya yake kama anamatatizo ya ugonjwa wa moyo au hana ni jambo la muhimu wasanii wote tukapime na kujua afya zetu.
“Nipende kutoa shukrani kwa Rais Samia Suluhu, Wizara ya Afya pamoja na Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Taasisi zake kwa kuunga mkono jambo hili la wasanii kucheki afya na kupatiwa matibabu.
Aidha Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu nchini Gerson Kasiga amesema kuwa wasanii fursa imejitokeza ni bure wanapaswa kuchangamkia na kujitokeza kuepuka magonjwa yasio ambukiza wajitokeze kupima moyo.
Naye Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) Kedmon Mapana amesema ni wakati wa wasanii kujitokeza kwa wingi kupatiwa matibabu na kuepuka magonjwa yasio ambukiza.