
MWANAMITINDO na Msanii wa muziki wa Bongo Fleva nchini, Miriam Odemba ameahidi kufanya vizuri kwenye tuzo za Zikoma zinazotarajia kufanyika Zambia mwishoni mwa mwezi ujao.
Akizungumza na gazet la HabariLEO, Odemba amesema kuwa ameingia kwenye tuzo hizo na wimbo wake wa Wema, ili kujitangaza kimataifa na watu wamjue kuwa ni miongoni mwa wasanii wa muziki na si mitindo pekee.
“Kwenye tuzo hizi nashiriki kwenye kundi la wasanii chipukizi lakini lengo ni kutaka nifahamike zaidi kimataifa lakini kwa hapa nyumbani siwezi kufanya hivyo kwa sababu tayari nina jina na ni mtu maarufu,” amesema Odemba.
Alisema ingawa anashiriki kwa mara ya kwanza kwenye tuzo hizo, lakini anaamini atafanya vizuri na kupeperusha vyema bendera ya Tanzania kutokana na ubora wa wimbo alioushindanisha.
Alisema anataka kuzitumia tuzo hizo, kama alama ya kujitambulisha na kuwaonesha waandaaji wa tuzo mbalimbali za kimataifa kuwa na yeye ni miongoni mwa wasanii waliopo kwenye muziki.
Msanii huyo amewaomba Watanzania kumpa sapoti kwa kumpigia kura kwenye tuzo hizo ambazo zaidi ya wasanii 80 kutoka Tanzania wanashiriki katika makundi mbalimba