Mastaa

Gigy Money amuomba msamaha Zuchu 

DAR ES SALAAM: MSANII wa muziki wa Bongo Fleva nchini, Gigy Money, amemuomba msamaha msanii mwenzake Zuchu kupitia ujumbe aliouandika kwenye ukurasa wake wa Instagram.

Katika ujumbe huo, Gigy Money alisema ameandika kwa moyo wa kweli na unyenyekevu akieleza kuwa anatamani kuweka mambo sawa kati yao.

“Natumaini uko salama na unaendelea vizuri. Nimechukua muda kuandika ujumbe huu kwa moyo wa kweli na unyenyekevu,” ameandika Gigy Money.

Aidha, msanii huyo alisema kuwa kama kuna sehemu yoyote alimkwaza au kumuumiza Zuchu, anaomba asamehewe kwa dhati.

“Kama kuna sehemu nilikuumiza au kukufanya ujisikie vibaya, naomba unisamehe kwa dhati kabisa. Siombi ili nirudishe yaliyopita kwa lazima, bali nataka moyo wangu uwe safi mbele yako na mbele ya Mungu,” ameongeza.

Mbali na ujumbe huo, Gigy Money amewataka mashabiki wake kutembelea ukurasa wake wa Instagram kusoma maelezo zaidi kuhusu ombi hilo la msamaha.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button