La Liga

Wachezaji muhimu kuikosa El Classico

MADRID: Mlinda mlango wa mabingwa wa kihistoria wa ligi ya mabingwa barani Ulaya Real Madrid, Thibaut Courtois atakosa mchezo wa El Classico wa Jumamosi hii kutokana na jeraha la misuli wa mguu wake wa kushoto

Uongozi wa klabu hiyo umeeleza katika taarifa yake iliyonukuu sehemu ya taarifa ya madaktari kuwa golikipa huyo amepata jeraha dogo ambalo litamfanya kukaa nje kwa muda kuanzia weekend hii.

“Kufuatia vipimo vilivyofanywa kwa mchezaji wetu Thibaut Courtois. Real Madrid Medical Services, imegundua amepatia na jeraha la misuli ya mguu wake wa kushoto.” imesema sehemu ya taarifa hiyo.

Mlinda mlango Namba mbili Andriy Lunin anatarajiwa kucheza dhidi ya Barcelona, ingawa mchezaji huyo wa kimataifa wa Ukraine ni kipa mzuri, kiwango kizuri cha Courtois kimekuwa kikimpa kile anachokihitaji meneja Carlo Ancelotti.

Real Madrid tayari itawakosa David Alaba, Rodrigo na Dani Carvajal kwa muda, na sasa kipa bora zaidi duniani atalazimika kukosa mchezo huo muhimu zaidi wa msimu huu.

Courtois amekuwa nguzo muhimu katika kikosi cha mabingwa hao akijihakikishia namba kwenye kikosi cha kwanza cha mabingwa hao watetezi wa ligi ya mabingwa barani Ulaya.

Related Articles

Back to top button