La Liga

Barcelona yaangukia pua kwa Olmo

BARCELONA: KIUNGO mshambuliaji wa FC Barcelona aliyesajiliwa hivi karibuni huenda asiendelee kuitumikia klabu hiyo baada ya mahakama jijini Barcelona kutupilia mbali rufaa ya FC Barcelona iliyopinga kuzuiwa na LaLiga kumsajili moja kwa moja Mhispania huyo.

Barcelona walimsajili Olmo mwezi Agosti kwa kitita cha takribani Euro milioni 55, lakini kutokana na klabu hiyo kushindwa kufikia kikomo cha mshahara cha LaLiga, kiungo huyo mshambuliaji alisajiliwa kwa kipindi cha nusu msimu pekee.

Usajili wa Olmo ulikuja baada ya majeraha ya muda mrefu kuwaweka nje wachezaji wa kikosi cha kwanza kwa miezi kadhaa, jambo ambalo liliruhusu Wakatalunya hao kutenga sehemu ya mishahara ya wachezaji hao majeruhi kumsajili mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26.

Olmo aliyeongoza Spain kutwaa kombe la Euro 2024 amekuwa sehemu muhimu ya Barcelona msimu huu, akiichezea michezo 15 na kuitunuku mabao 6 na asisti 1. Barça wapo nafasi ya 3 katika msimamo wa ligi wakiwa nyuma ya vinara Atletico Madrid kwa pointi 3

Related Articles

Back to top button