Kuogelea

Wachezaji kuogelea waboresha muda

BUDAPEST:WAOGELEAJI wanne waliokwenda kushiriki mashindano ya kuogelea ya Dunia wameboresha muda wao katika mashindano hayo yanayoendelea mjini Budapest nchini Hungary.

Kwa mujibu wa Kocha Mkuu wa timu hiyo Alex Mwaipasi, Aliyana Kachra ameogelea mita 100 katika mtindo wa backstroke siku ya kwanza na kupunguza muda wa sekunde 3.2.

Aidha, Michael Joseph pia ameogelea jana mita 50 Butterfly akimaliza na muda wa sekunde 28.51.

Kwa upande wa Lina Goyai amepunguza muda wake kwa sekunde moja kwenye mita 100 Freestyle huku Collins Saliboko naye akipunguza muda wake kwa sekunde 1.74 kwenye mita 100 Freestyle.

Kocha Mwaipasi amesema kuna changamoto kidogo hasa hali ya hewa kwani wametoka kwenye joto Dar es Salaam wamekwenda kwenye baridi kidogo lakini haijaathiri viwango vyao.

Amesema “ kila mtu amebakiza mchezo mmoja, vijana wamefanya vizuri, wamepiga hatua kwa kuboresha muda wao kwetu sisi tunaona ni mafanikio, kuna changamoto ndogo na kubwa ni hali ya hewa, japo kimchezo haituathiri sana”.

Related Articles

Back to top button