Kuogelea

Waogeleaji 49 tayari kuchuana Kanda ya 3

DAR ES SALAAM: Waogeleaji 49 na viongozi tisa wameanza safari kuelekea nchini Burundi kushiriki mashindano ya Afrika kanda ya tatu huku Baraza la Michezo la Taifa (BMT) likiwahimiza kuwakilisha vizuri.

Mashindano hayo yanatarajia kuanza Ijumaa na kuhitimishwa Jumapili.

Akizungumza Dar es Salaam katika hafla ya kuagwa kwa timu hiyo ya taifa Ofisa Michezo wa wa BMT, Charles Maguzu amewataka waogeleaji hao watumie mashindano hayo kuliheshimisha Taifa.

“ Hakikisheni mnashindana kwa mioyo mmoja huku mkiwa na kumbukumbu kuwa mnalipambania taifa kama wapiganaji kulinda heshima ya taifa letu,”alisema.

Maguzu ameishukuru kampuni ya Great lake zone kwa kugharamia gharama za timu hiyo kuelekea nchini Burundi huku akisema hatua hiyo ni namna mojawapo ya kuiunga mkono serikali katika jitihada zake za kuinua michezo nchini.

Kocha Mkuu wa timu hiyo Michael Livingstone amesema kuwa maandalizi ya kikosi hicho yako vizuri kwani wamekuwa wakijifua kwa muda mrefu kwaajili ya mashindano hayo ambayo anaamini kuwa ushiriki wao utaliheshimisha taifa.

Nahodha wa timu hiyo Colins Saliboko ameahidi watarejea na ushindi akisema maandalizi waliyoyapata kutoka kwa benchi la ufundi yanawapa nafasi ya kujiamini.

Related Articles

Back to top button