Rais kumtunuku tuzo aliyepeleka medali ya dhahabu Pakistan

LAHORE: MSHINDI wa medali ya dhahabu kwa kurusha mkuki umbali mrefu, Arshad Nadeem raia wa Pakistan kutua nchini humo na medali ya dhahabu, Rais wa nchi hiyo, Asif Ali Zardari ametangaza siku ya Jumamosi kwamba shujaa huyo atatunukiwa tuzo ya kiraia ya pili kwa juu zaidi Pakistan, Hilal-i-Imtiaz, kutokana na mafanikio aliyoyapata kwake nan chi ya Pakistan.
Medali hiyo inakuwa ya kwanza ya dhahabu kwa nchi hiyo baada ya miaka 40. Nadeem alipokelewa kishujaa na idadi kubwa ya wapakistan kisha baba yake alimvisha shada la maua shingoni mwake huku maelfu ya wananchi waliofika kumpokea shujaa huyo wakiimba nyimbo za pongezi, “Uishi Muda Mrefu Arshad Nadeem! Uishi Muda Mrefu Pakistani!”.
“Ninamshukuru Mungu Mwenyezi. Nawashukuru wazazi wangu na taifa la Pakistani,” Nadeem aliuambia umati. “Kuna kazi ngumu sana kwangu na kocha wangu Salman Butt lakini tumeshinda ndiyo jambo la kufurahia.”
Arshad mwenye miaka 27 ni baba wa watoto wawili alimshinda bingwa mtetezi Neeraj Chopra ambaye anatoka nchi Jirani ya India.
Arshad alirusha mkuki urefu wa mita 92.97 ambapo aliweka rekodi katika mashindano hayo ya Olimpiki ambapo mtupo huo umekuwa ni rekodi ya sita bora kuwahi kutokea katika mashindano hayo toka yaanzishwe.
Mmoja wa waliompokea shujaa huyo ni Mohammad Farooq aliyesafiri kwa saa nyingi kutoka mji wa Sargodha Kwenda Sahare kumpokea mshindi huyo.
“Nimekuja hapa… kumkaribisha shujaa wetu. Pakistan imepata furaha baada ya miaka 40. Imekuwa furaha kubwa zaidi kwani Agosti 14 ndiyo siku ya sherehe za uhuru wetu,” alisema.