Afrika Mashariki
Vipers kibaruani UPL
VIWANJA vitatu vitatimka vumbi leo wakati timu sita zitakapomenyana kusaka pointi muhimu katika mfululizo wa Ligi Kuu Uganda(UPL).
Miamba ya Uganda, Vipers itakuwa uwanja wa nyumbani wa St. Mary’s katika jiji la Entebbe kuikaribisha Bright Stars.
Kwenye uwanja wa Mehta uliopo mji wa Lugazi, Maroons itakuwa mgeni wa URA wakati Busoga United itaikaribisha Gadaffi kwenye uwanja wa uwanja wa kituo cha ufundi cha FUFA kilichopo mji wa Njeru.
Kitara inaongoza UPL yenye timu 16 ikiwa na pointi 39 baada ya michezo 19 wakati Arua Hill inaburuza mkia ikiwa na pointi 5 baada ya michezo 15.