Afrika Mashariki

Ni Tanzania vs Uganda U18 leo

TIMU ya taifa ya soka Tanzania kwa wasichana wenye umri chini ya miaka 18 inashuka dimbani leo kuikabili Uganda katika michuano ya Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati(CECAFA) inayoendelea Dar es Salaam.

Mchezo huo utakaofanyika uwanja wa Azam Complex utatanguliwa na mchezo kati ya Zanzibar na Burundi.

Tayari Tanzania imecheza michezo mitatu ya michuano hiyo ikizifunga Burundi 3-0, Ethiopia 2-0 na Zanizbar 1-0.

Uganda inaongoza kwa kuwa na idadi kubwa ya magoli ikilingana na Tanzania katika pointi 9, Ethiopia pointi 6 huku Zanzibar na Burundi hazina pointi.

Related Articles

Back to top button