Van Dijk: hakuna kinachoendelea mimi na Liverpool

LIVERPOOL, Beki wa Liverpool Virgil van Dijk amethibitisha kuwa mpaka sasa hakuna maamuzi yeyote yaliyothibitishwa na uongozi wa Liverpool juu ya hatma ya mchezaji huyo kuendelea kusalia klabuni hapo au kupewa mkono wa kwaheri.
Van Dijk amenukuliwa akisema yeye hafahamu kama uongozi wa Liverpool una mpango wowote wa kumbakisha Anfield na hajui pia kama utamruhusu kuondoka mkataba wake utakapotamatika mwishoni mwa msimu huu.
“Bado sijui ni nini kitatokea msimu ujao, kama kuna mtu anakwambia anajua basi anakudanganya. Mkataba mezani? Hakuna kitu kama hicho na mara zote nimekuwa nikiwaambia hili na kama kuna habari yeyote mpya mtajua tuu. Najua mnajua kuna mazungumzo yanaendelea chini chini lakini ni hivyo tu” amesema
Tayari taarifa mbalimbali zimekuwa zikimhusisha beki huyo raia wa Nederlands na timu kadhaa kubwa ikiwemo tetesi za hivi karibuni za kuhusishwa na PSG baada ya kuonekana akizungumza na rais na mmiliki wa mabingwa hao wa Ufaransa Nasser A-Khelaifi,