EPL

Mwanzo mpya United na Ruben Amorim

MANCHESTER: KLABU ya Manchester United imemthibitisha Ruben Amorim kama kocha wao mpya baada ya tetesi za muda mrefu.

Amorim raia wa Ureno anachukua nafasi ya mtangulizi wake aliyefutwa kazi mwezi uliopita Erik ten Hag, baada ya mashetani hao wekundu kulipa kiasi cha pauni milioni 10 (£8.4m) kumleta Old Trafford.

Taarifa iliyotolewa na klabu hiyo imesomeka: “Manchester United ina furaha kutangaza uteuzi wa Ruben Amorim kama Kocha Mkuu wa kikosi cha kwanza cha wanaume,”

“Atakuwa nasi hadi Juni 2027 na uwezekano wa kuongeza mwaka mmoja mara tu atakapokuwa ametimiza wajibu wake kwa klabu. Atajiunga na timu yetu jumatatu, 11 Novemba.”

Ruben mwenye miaka 39 ni mmoja wa makocha wa kizazi kipya wenye viwango vya juu katika soka la Ulaya. Akisifiwa sana kama mchezaji na kocha, mataji yake ni pamoja na kushinda Ligi Kuu ya Ureno mara mbili akiwa na Sporting CP, la kwanza likiwa ni kombe la kwanza kwa klabu hiyo katika miaka 19.

Amorim anakuwa kocha wa 10 kuifundisha klabu hiyo tangu kuondoka kwa Sir Alex Ferguson Ferguson. Maswali ya wadau wengi wa soka ni je!, Ruben atautafuna mfupa uliomshinda Erik ten Hag?

Related Articles

Back to top button