EPL
Wolves wavunja kitasa cha Reims

LONDON, England: Klabu ya Wolves ya England imefanikiwa kunasa saini ya beki wa Reims inayoshiriki ligi kuu ya Ufaransa Ligue 1 Emmanuel Agbadou kwa mkataba wa muda mrefu wa miaka minne na nusu.
Vyombo vya habari nchini England vimeripoti kuwa uhamisho huo wa Agbadou umeigharimu Wolves kitita cha zaidi dola milioni 20.3 ambazo ni karibu shilingi bilioni 50 za kitanzania.
Raia huyo wa Ivory Coast mwenye miaka 27 anakuwa mchezaji wa kwanza wa meneja mpya wa Wolves Vitor Pereira anaepambana kuboresha eneo lake la ulinzi ambalo limeonekana kuvuja sana msimu huu
Wolves wanapiga deki katika nafasi ya 17 ya msimamo wa ligi kuu ya England wakiwa na points 16 sawa na Ipswich Town walio katika mstari wa kushuka daraja.