Uwoya: Mungu alituongoza Korea
DAR ES SALAAM: Mrembo na mwizaji wa Filamu nchini ambaye pia ni mtumishi wa Mungu Irene Uwoya amesema ameongozwa na Roho Mtakatifu kutoka nchini South Korea hadi aliporudi Tanzania
Amesema hatua ya Rais Samia kuwapeleka wasanii nchini Korea amefungua masoko ya Filamu kimataifa sio jambo la kawaida.
Amesema kuwa “Nilipokuwa NchiniKorea nimejifunza kuwa ni Mungu ametuongoza wasanii wa Tanzania tukajifunze sio kawaida.”
Pia ameongeza kuwa anamshukuru Mungu kuanzia mwanzo wa safari hadi mwisho, waliongozwa na Roho Mtakatifu hadi kurudi nchini na wamejifunza mazuri ya kuyafanya nchini.
“Wasanii wa Korea wanajali maudhui ya Filamu zao hakuna maudhui ya kutoka nje ya Nchi hiyo yanayoruhusiwa kutoka kwenye Filamu zao zaidi ya wao wenyewe.
“Kumekuwa na vyuo vya kuwajengea uwezo wasanii wa Filamu na na mfuko wakusadia wasanii wa Filamu, katika kila nyanja.”amesa Irene Uwoya.