Filamu

‘Hemed PHD’, Lulu Diva wayamaliza

DAR ES SALAAM: TAMTHILIA ya ‘Nice to Meet you’ inayowakutanisha waigizaji Lulu Abas ‘Lulu Diva’ na Hemed Suleiman ‘Hemed ‘PHD’ waliokuwa na uhasama imezinduliwa rasmi na kuwafanya wao kumaliza tofauti zao.

Wawili hao inasemekana walianza tofauti zao tangu walipokuwa lokesheni wakirekodi Tamthilia hiyo iliyowahusisha na ugomvi wao kuendelea hadi kwenye maisha yao ya kawaida.

Lakini wawili hao wameombana msamaha na kuendelea na maisha yao baada ya kumaliza tofauti zao hizo.

Akizungumza na waandishi wa habari Hemed PHD alisema kuwa yeye ndio aliyebeba thamthilia hiyo ya ‘Nice to meet you’ itakayo kuwa inarushwa Startimes kupitia chanel ya Swahili Plus.

“Ushiriki wangu katika tamthilia hii Mimi ndio muhusika Mkuu na nimeigiza kama mtumishi wa Mungu nimeigiza humo ndo unatakiwa kumfatilia kuanzia uzinduzi rasmi hadi tamthilia yenyewe Watanzania wajiandae kumuona Saimon Mlokole.

“Natoa shukrani zangu kwa wote tulioshirikiana ni tamthilia yenye visa na matukio mengi na mafundisho katika jamii yetu ya Tanzania,”amesema Hemed PHD.

Kwa upande wa Lulu naye pia, amesema hakutaka kupishana na Hemed lakini ni tofauti za kibinadamu wao kupishana alioneshwa kuchukukizwa lakini kwa sasa wapo sawa watu wafatilie tamthilia hiyo.

“Nice to meet you ni mradi mzuri, kazi nzuri watu wataipenda, tumeigiza vitu vingi,”amesema. Wasanii wote wawili wameigiza kama wahusika wakuu kwenye tamthilia hiyo.

Naye Mkurugenzi wa Masoko na Maudhui wa Startimes David Malisa amesema tamthilia hiyo imeshaanza kurushwa rasmi kupitia Chanel ya Swahili Plus.

Amesema ndani ya tamthilia hiyo kuna kisasi, mapenzi, maisha ya hali ya chini na kwamba ni tamthilia itakayoshika hisia za kila mtu kutokana na ujumbe uliko ndani yake.

Related Articles

Back to top button