Ukumbi wa Dolby unaotumika kwa tuzo za Oscars wapata bosi mpya
KAMPUNI ya uwekezaji ya Jebs Hollywood Entertainment, imenunua ukumbi maarufu wa michezo ya jukwaani Dolby kwa takriban dola milioni 50 na tayari wameshamtangaza mmiliki mpya wa ukumbi huo maarufu unatumika wakati wa utoaji wa tuzo za Oscars.
Kampuni hiyo, ambayo ilinunua ukumbi huo inamilikiwa na Mtayarishaji wa sinema Elie Samaha na Rais wa zamani wa Sony Pictures Entertainment Jeff Sagansky.
Jebs Hollywood Entertainment pia inaendesha Ukumbi wa Michezo ya Jukwaani wa Kichina wa TCL.
Mkurugenzi mkuu wa Avison Young, Chris Bonbright, katika taarifa yake amesema sherehe za tuzo za Oscar ziliandaliwa tangu mwaka 2001, katika ukumbi huo wa michezo wa Dolby wenye viti 3,400. Wamiliki wapya wanakusudia kuendeleza utamaduni huo huku wakionyesha shughuli nyingine mbalimbali.
Ukumbi huo wa Dolby unajumuisha sehemu ya kupaki magari inayojulikana kama Hollywood & Highland. Pia kuna eneo la maegesho ya magari yenye ukubwa wa ekari 1.45, kulingana na Avison Young ambayo ni kampuni ya mali isiyohamishika.