Filamu

Mimi Mars arejea kivingine

DAR ES SALAAM: MSANII wa Bongo Fleva, Marianne Mdee maarufu Mimi Mars amesema kwa sasa ameruhisiwa na daktari wake kuendelea na shughuli zake za sanaa na muziki zilizosimama kwa muda mrefu baada ya kupata ajali ya gari.

Msanii huyo aliyetamba kwenye tathmilia ya Jua Kali akiigiza kama Maria au Mwanakondoo, alipata ajali mapema mwezi Januari na kusababisha nafasi yake katika tamthilia hiyo kuchukulia na Elizabeth Michael ‘ Lulu’.

Akizungumza jijini Dar es Salaam Mimi Mars amesema amesema kuwa kwa sasa amerudi rasmi katika Tasnia ya Filamu.

“Kwa sasa nipo sawa na nimeruhusiwa na daktari wangu aliyekuwa akinipatia matibabu baada ya kupata ajali na nimerudi rasmi nitakuwa nikionekana katika tamthilia ya Njia niliyocheza kama Binti wa kimasai niliyesoma nje ya nchi.”

“Niliporuhusiwa Mzalishaji wa tamthilia ya Njia alinifata tukakunaliana nikalizika na malipo ni mazuri tofauti na nilivyokuwa nikilipwa awali nadhani hii ni baada ya kuona na kuwa na imani na kipaji changu”amesema Mimi Mars

Pia ameongeza kwa kuwataka mashabiki zake kuendelea kumfatilia kwa kuwa amefanya Kazi nzuri kama mnavyomjuwa hajawai kuwa na kazi mbovu.

Kwa upande wake Rukhsaar Vazda maarufu kama Jiya amemkaribisha Mimi Mars na kumpongeza kuwa ni msanii mwenye nidhamu.

Naye Breena Pinto (Jaya) ambaye anacheza kama mpenzi  wa Mimi Mars kwenye tamthilia ya Njia amesema kuwa katika tamthilia hiyo wamekuwa wakishindana nani mkali.

 

Related Articles

Back to top button