Kwingineko

UEFA yakomba mabilioni ya Chelsea

SHIRIKISHO la soka barani Ulaya UEFA limeipiga faini ya euro milioni 31 ambazo ni sawa na shilingi bilioni 96.4 za Kitanzania kwa kukiuka sheria zake za kifedha, huku Aston Villa, Barcelona na Olympique Lyonnais pia zikitozwa faini kubwa.

Adhabu hizo zinaambatana na uwezekano wa kutozwa faini kali zaidi huku Chelsea, ambao walikubali afueni ya miaka minne na Bodi ya Udhibiti wa Kifedha wa Klabu ya UEFA (CFCB), wakiwa katika hatari ya kupigwa faini ya hadi euro milioni 60 zaidi ikiwa hawatapanga hesabu zao vizuri.

FC Barcelona watalazimika kulipa faini ya euro milioni 15, lakini wanaweza kukabiliwa na kiwango kikubwa kinachoweza kufikia euro milioni 60 kwa jumla, huku UEFA pia ikiitoza klabu ya Lyon ya Ufaransa euro milioni 12.5 na Aston Villa euro milioni 11.

Chelsea wametozwa euro milioni 20 kwa kutofuata sheria ya mapato ya soka na euro milioni 11 kwa kukiuka sheria ya gharama ya kikosi, huku Aston Villa wakitozwa faini ya euro milioni tano na milioni sita kwa kukiuka sheria zao.

Klabu hizo pia zimewekewa vikwazo vya usajili wa wachezaji wapya kwenye kikosi A cha mashindano ya klabu ya UEFA kama vile Ligi ya Mabingwa barani Ulaya na Europa League.

Related Articles

Back to top button