Uchebe: Nampenda Shilole, siyo adui yangu

DAR ES SALAAM: MPENZI wa zamani wa Msanii Zuwena Mohamed ‘Shilole’ Uchebe ameweka wazi kuwa hana chuki na aliyekuwa mpenzi wake, Shishi, akieleza kuwa kuachana siyo vita ndiyo maana wakikutana husalimiana kwa heshima na upendo.
Kuhusu uhusiano wao wa sasa, Uchebe amesema bado wanaheshimiana licha ya kuachana.
“Salamu ni vizuri, mimi sina chuki na mtu. Tumeachana kwa wema,” amesema Uchebe.
Mbali na hilo, Uchebe pia amezungumzia ukaribu wake na Esma Platnumz, dada wa msanii Diamond Platnumz, baada ya kuzuka kwa taarifa mbalimbali kuhusu wawili hao kuwa kwenye mahusiano ya kimapenzi.
Uchebe amekanusha madai hayo na kusisitiza kuwa yeye na Esma wana uhusiano wa kindugu na heshima kubwa.
“Mimi yule Esma ni dada yangu, ni mtu ambaye ninaheshimiana naye sana na ninampenda sana,” amesema Uchebe.




