Mahusiano

Aamir Khan aajiri mlinzi kwa mpenzi wake

Ataka kukwepa wanahabari

MUMBAI : KATIKA hali ya kushangaza muigizaji maarufu nchini India, Aamir Khan ameajiri mlinzi binafsi wa kumlinda mpenzi wake Gauri Spratt na waandishi wa Habari walioanza kumfuatilia mara tu baada ya kuweka wazi uhusiano wao.

Aamir Khan amesema mlinzi huyo atakuwa na kazi ya kumlinda mpenzi wake kutokana na purukushani za waandishi wa habari wanaomfuatilia kutaka kujua Habari mbalimbali kumuhusu yeye na familia yake.

Aamir alimtambulisha Gauri Spratt kwa vyombo vya habari katika Hoteli ya Mumbai jana Machi 13 na mara baada ya kumtambulisha mpenzi wake huyo anayeishi Bangalore waandishi wote walianza kumuandama kwa maswali mwanamke huyo.

“Nimejaribu kumwambia jinsi itakavyokuwa, usumbufu wa vyombo vya habari, na kumuandaa kwa kiasi fulani kwa hilo. Hajazoea hilo. Lakini tunatumai kuwa nyinyi mtakuwa wema kwake,” Aamir aliwaambia wafanyakazi wa vyombo vya habari kwenye mkusanyiko huo.

Gauri Spratt na Aamir wamekuwa wakichumbiana kwa miezi 18 sasa.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button