Habari Mpya

Twiga Stars kujipima na Morocco

MOROCCO: KIKOSI cha timu ya taifa wanawake Twiga Stars kipo nchini Morocco kujiandaa na michezo miwili ya kirafiki kwa mujibu wa kalenda ya FIFA

Mchezo wa kwanza ni dhidi ya Morocco utakaochezwa October 25 na mchezo wa pili utachezwa Oktoba 27 dhidi ya Senegal. Baada ya michezo hiyo watarejea katika klabu kuendelea na majukumu.

Kocha Mkuu wa timu hiyo, Hilda Masanche amesema wachezaji wote wamewasili hata wale wanaocheza soka nje, maandalizi yanaenda vizuri kwa ajili ya michezo hiyo ya kirafiki.

“Wachezaji wote wapo kambini na tunaendelea kufanya maandalizi hapa Morocco kwa ajili ya michezo miwili dhidi ya wenyeji wetu pamoja na Senegal,” amesema.

Hilda amesema muhimu ni kupata matokeo katika michezo hiyo ambayo ipo kwenye kalenda ya FIFA, michezo hiyo itawaongezea wachezaji kujiamini na kupanda katika viwango.

 

Related Articles

Back to top button