Ligi Daraja La Kwanza

‘Tulsa King’ atarejea na msimu wa 3 na 4

NEW YORK: Mashabiki wa tamthilia maarufu ya uhalifu ‘Tulsa King’, inayoongozwa na mtaalamu wa filamu za mapigano na vita, Sylvester Stallone ‘Rambo” wametangaziwa kupata msimu wa tatu na nne wa tamthilia hiyo ambayo kwa sasa inabamba ikiwa katika msimu wake wa pili.

Taarifa za tamthilia hiyo zimenathibitisha kuwa kipindi hicho, ambacho kilioneshwa kwa mara ya kwanza kwenye Paramount+ mwaka wa 2022, kitarejea kwa misimu yote miwili ya 3 na 4 hivi karibuni.

Katika tamthilia hiyo Stallone Rambo ndiye muongozaji wa tamthilia hiyo na pia ameigiza kama Dwight ‘The General’ huku   Manfredi akihudumu kama mtayarishaji mkuu wa tamthilia hiyo.

Mashabiki wa tamthilia hiyo wana mengi ya kutazamia kufuatia mtiririko wa mwisho wa Msimu wa 2 wa tamthilia hiyo huku mfululizo ukiwa na mafanikio makubwa kutokana na kuvutia kwa hadithi yake lakini pia umaarufu na nguvu ya nyota ya Stallone Rambo.

Kulingana na Movieweb, kuna mazungumzo hata ya kupanua kipindi zaidi, ikiwezekana na mabadiliko, sawa na ubunifu mwingine wa Taylor Sheridan, kama vile ‘Yellowstone’.

Wadadisi wa mambo ya ndani wanadokeza kuwa ‘Tulsa King’ inaweza kukua zaidi ya misimu yake ijayo. Inaripotiwa kuwa timu inachunguza wapi pa kuongeza ili kuendelea kuimarika kimataifa.

Kulingana na Movieweb, malipo ya Sylvester Stallone pia yameona ongezeko kubwa kadiri kipindi kinavyopata umaarufu. Kwa msimu wa kwanza, tamthilia hiyo ilipata dola za Marekani750,000 kwa kila kipindi, ambayo iliongezeka maradufu hadi dola za Marekani 1.5 milioni kwa Msimu wa 2.

Tamthilia hiyo kupitia mfululizo huo umevuta watazamaji zaidi ya milioni 10 duniani kote kwa msimu wa pili ikiwa ni ongezeko la asilimia 8 kutoka msimu wa kwanza.

Uamuzi wa Paramount wa kupeperusha msimu wa 2 kwenye CBS, umesaidia kuvutia watazamaji wapya. Vipindi vyote tisa vilitangazwa kwenye cable TV na kutambulisha kipindi kwa watu ambao huenda hawakujisajili kwenye mtandao wa Paramount+.

Rambo kupitia ukurasa wake wa Instagram amedokeza kwamba  msimu mpya wa ‘Tulsa King’ kwa mashabiki wake na kuzjizolea jumbe nyingi za kupongeza huku naye akiwashukuru mashabiki wake.

Related Articles

Back to top button