Mastaa

Tems awekeza pesa kwenye timu ya Ligi Kuu Marekani

CALIFORNIA: MWIMBAJI na mtunzi wa nyimbo kutoka nchini Nigeria Tems amekuwa mmiliki rasmi wa timu ya Ligi Kuu ya Soka (MLS), San Diego FC (SDFC), kupitia kampuni yake ya The Leading Vibe.
Uwekezaji wake, uliofanywa kwa ushirikiano na Pave Investments,kampuni binafsi ya uwekezaji barani Afrika unaashiria nyongeza muhimu kwa kundi la umiliki wa kilabu hiyo.

Akielezea furaha yake, Tems amesema, “Nimefurahi kujiunga na kikundi cha umiliki cha San Diego FC na kuwa sehemu ya klabu inayosherehekea ubunifu, utamaduni, na jumuiya. Kandanda huwaunganisha watu kwa njia ya nguvu, na nina hamu ya kusaidia kujenga kitu maalumu huko San Diego.

Tems anajiunga na kundi mashuhuri la wamiliki wa timu hiyo, ikiwa ni pamoja na mwigizaji na mtayarishaji Issa Rae, mwanasoka wa zamani wa Uhispania Juan Mata, mstaafu wa Jeshi la Wanamaji la Marekani Jocko Willink, na nyota wa MLB Manny Machado.

Kujitosa kwa Tems katika umiliki wa michezo kunaangazia mwelekeo unaokua wa watu mashuhuri wanaowekeza katika umiliki wa michezo. Mifano mashuhuri ni pamoja na Ryan Reynolds na Rob McElhenney wakiwa na Wrexham AFC, LeBron James akiwa na Liverpool FC, Ed Sheeran akiwa na Ipswich Town na Serena Williams akiwa na Angel City FC.

Tems mwezi huu wa pili ameshinda Tuzo yake ya pili ya Grammy, na kupata kutambuliwa kwa wimbo wake ‘Love Me JeJe.’ Hapo awali, alishinda Grammy kwa ushirikiano wake kwenye Future ‘Wait for U’.

Related Articles

Back to top button