Mastaa

Lady Gaga amtangaza mtaalamu wa teknolijia kuwa mchumba wake

PARIS: MWANAMUZIKI wa Kimarekani mwenye vituko lukuki Lady Gaga amemtangaza rasmi mchumba wake Michael Polansky ambaye ni mtaalamu wa teknolojia.

Lady Gaga na Michael wanadaiwa kuwa katika uhusiano na uchumba kwa muda mrefu huku wote wakionekana kufurahia mahusisno yao ya sasa.

Lady Gaga mwenye miaka 38 alimtambulisha mchumba wake huyo kupitia mtandao wa TikTok wakati alipokuwa akizungumza na Waziri Mkuu wa Ufaransa Gabriel Attal kwenye Michezo ya Olimpiki ya 2024 huko Paris, Ufaransa.

Katika video hiyo ya Tiktok Lady Gaga anaonekana akiwa amevalia koti la mshambuliaji wa timu ya Marekani na miwani ya jua yenye mkia wa farasi unaoteleza, akizungumza na mwanasiasa huyo kuhusu michezo ya Olimpiki 2024 ndipo akamtaja mchumba wake huyo mwenye miaka 46

Related Articles

Back to top button