Ligi Daraja La Kwanza

Tatjana Maria adai amekossewa heshima na waandaaji

LONDON:BINGWA mtetezi wa mashindano ya Queen’s Club, Tatjana Maria wa Ujerumani, amesikitishwa na uamuzi wa waandaaji wa mashindano hayo kutompa mwaliko wa moja kwa moja (wildcard), hali iliyomlazimu kucheza mechi za mchujo ili kufuzu hatua kuu.

Maria, ambaye mwaka jana aliandika historia kwa kutwaa ubingwa wa wanawake katika klabu hiyo baada ya miaka 52 tangu mashindano hayo kufanyika kwa wanawake, alisema alitarajia kupewa nafasi ya moja kwa moja kama ishara ya kuthamini mafanikio yake.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 37 alisema alishangazwa kuona waandaaji wakitoa kadi maalum kwa wachezaji wa nyumbani huku yeye akilazimika kuanza safari ya utetezi wa taji kupitia hatua ya mchujo.

“Nadhani mabingwa watetezi wanapaswa kupewa heshima zaidi. Nilitarajia kupata mwaliko wa moja kwa moja,” alisema Maria.

Licha ya changamoto hiyo, Kwa Maria amefanikiwa kufuzu hatua kuu na anatarajiwa kukutana na Maria Sakkari wa Ugiriki katika raundi ya kwanza ya mashindano hayo

Related Articles

Back to top button