Ligi Daraja La Kwanza

UNITED, Gunners wamtaka Xavi, PSG wanabana

ARSENAL na Manchester United ni miongoni mwa klabu zinazopigania huduma ya Mholanzi Xavi Simon anayekipiga RB Leipzig ya Ujerumani kwa mkopo.

Taarifa iliyoripotiwa na mtandao wa Sky Sport ukiunukuu mtandao wa L’Equipe imeeleza klabu hizo zimewasiliana na Paris Saint Germain ambao ndio wamiliki wa mchezaji huyo kuhusu uwezekano wa kumsajili katika dirisha hili.

Taarifa hiyo imeeleza Bayern Munchen pia imeonesha dhamira ya kutaka saini ya kiungo huyo wa pembeni, licha ya ripoti kuwa PSG hawana mpango wa kumuuza.

Sky Sport wameripoti kuwa PSG inapanga kubaki na nyota wao hata hivyo wana mpango wa kumtoa tena kwa mkopo msimu mwingine.

Akiwa na RB Leipzig kwa mkopo, Simons alifunga mabao 10 na kutoa pasi za mabao 15 msimu uliopita.

Miaka kadhaa nyuma akiwa PSV ya Uholanzi, Arsenal iliwahi kuhusishwa kutaka saini ya mchezaji huyo ambaye kwa sasa yupo katika majukumu ya timu ya taifa kwenye mashindano ya Euro2024.

Related Articles

Back to top button