Hakuna mashabiki wanaowazidi hawa kwa sasa

NEW JERSEY:BAADA ya kusubiri kwa miaka 24 kurejea Kombe la Dunia, timu ya taifa ya Norway imehakikisha nafasi yake katika hatua ya mtoano na kuendelea kuwa moja ya timu zinazovutia mashindanoni humo.
Mbali na ushindi wao uwanjani, mashabiki wa Norway wamevutia macho ya dunia kwa shangwe maarufu ya “Viking Row”, ambayo imekuwa moja ya sherehe zinazozungumziwa zaidi katika Kombe la Dunia 2026.
Katika Uwanja wa MetLife, maelfu ya mashabiki walionekana wakifanya shangwe hiyo kwa pamoja huku wakiiunga mkono timu yao kwa nguvu kubwa.
Picha na video za mashabiki hao zimeenea duniani kote, huku wengi wakitaja “Viking Row” kama moja ya matukio bora ya mashabiki katika mashindano haya.
Norway imefuzu hatua ya mtoano, na pamoja na sapoti kubwa kutoka kwa mashabiki wao, matumaini ya kufanya vizuri zaidi yanaendelea kuongezeka.




