Nyumbani
Mmeiona Simba ya ubaya Ubwela?
DAR ES SALAAM: SIMBA imewafunga midomo wale ambao walikuwa wakiibeza baada ya kushinda mabao 2-0 katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya APR FC.
Bao la kwanza lilifungwa na Debora Fernandez huku bao la pili likifungwa na Edwin Balua katika dakika ya 66 kwa mpira wa adhabu wa moja kwa moja uliomshinda kipa wa APR
Kocha Mkuu wa Simba, Fadlu Davids amejaribu kikosi chake kwa kila mchezaji kumpa nafasi ya kucheza katika mchezo huo wa kilele cha Simba day.