
LIGI Kuu ya soka Tanzania Bara inaendelea leo kwa mchezo mmoja wa miamba ya soka Simba na Azam ya Dar es Salaam.
Azam ni mwenyeji katika mchezo huo katika uwanja wa Benjamin Mkapa.
Simba inashika nafasi ya 3 katika msimamo wa ligi ikiwa na pointi 14 baada ya michezo 6 wakati Azam ipo nafasi ya 9 ikiwa na pointi 11 baada ya michezo 7.
Katika mchezo wa mwisho kukutana msimu wa 2021/22 Mei 18, 2022 timu hizo zilitoka sare ya bao 1-1.
Michezo miwili ya ligi hiyo imepigwa Dar es Salaam Oktoba 26 ambapo Yanga imeendeleza rekodi ya kutofungwa michezo 44 baada ya kuifunga KMC bao 1-0 katika uwanja wa Benjamin Mkapa huku Geita Gold ikipata ushindi wa mabao 2-1 katika uwanja wa Uhuru.