Ligi Ya Wanawake

Tanzania wenyeji wa mashindano ya GIFT

DAR ES SALAAM: TANZANIA inatarajia kuwa mwenyeji wa mashindano ya kwanza ya CAF ya Wasichana U 17 Integrated Football Tournament (GIFT) yaliyoandaliwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika.

Mashindano hayo ya Kihistoria yatafanyika Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam kuanzia Januari 7 hadi 18 2025 kwa kuzikutanisha timu nane kutoka kwenye Vyama Wanachama wa CECAFA (Mas).

Mpango wa mashindano hayo kukuza maendeleo ya soka ya wanawake barani Afrika na yanatoa jukwaa la kuonesha wanasoka wachanga wa kike, kujenga uwezo wa wachezaji na kukuza soka la wanawake katika ngazi za kikanda na bara.

Mashindano hayo ni sehemu ya mkakati wa CAF wa kukuza usawa wa kijinsia na kuwezesha kizazi kijacho cha wanasoka wa kike.

CAF imedhamiria kuongeza ushiriki wa wasichana katika soka barani kote, kuhimiza klabu kuwekeza katika vilabu vya soka vya wasichana, ligi na timu za taifa za wanawake chini ya umri wa miaka 17, kutoa njia kwa wasichana kuhama kutoka mpira wa shule kwenda kwa mpira wa ushindani.

Related Articles

Back to top button