Ligi Ya Wanawake
Kipa Simba Queens ndo basi tena
DAR ES SALAAM: SIMBA Queens imepata pigo kubwa la kukosa huduma ya kipa wa timu hiyo Coraline Rufa ambaye atakuwa nje ya uwanja kwa msimu mzima baada ya kufanyiwa upasuaji wa goti.
Rufa raia wa Kenya alipata jeraha hilo katika mchezo wa nusu fainali ya michuano ya CECAFA dhidi ya Kenya Police Bullets iliyofanyika nchini Ethiopia, Agosti 2024.
Daktari wa Simba, Naima Mohammed amesema upasuaji huo unamfanya kipa huyo kukaa nje ya uwanja kwa miezi nane kabla ya kurejea dimbani na kukosa msimu huu wote wa Ligi ya Wanawake Tanzania.
“Upasuaji umeenda vizuri na matarajio yetu ni kwamba baada ya kupona atakuwa tayari kurudi uwanjani kuendelea na majukumu yake ya kutumikia klabu ya Simba kwa msimu mwingine” amesema Naima.