Ligi Ya WanawakeNyumbani
Ni vita JKT vs Simba Ligi Kuu wanawake
LIGI Kuu ya mpira wa miguu kwa wanawake inaendelea leo kwa michezo mitatu kwenye viwanja tofauti.
Mchezo kivutio ni kati ya JKT Queens itakayochuana na Simba Queens kwenye uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo, Dar es Salaam.
Katika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma, Geita Gold Queens itakuwa mgeni wa Baobab Queens wakati Amani Queens itakuwa wenyeji wa Alliance Girls.